Jumanne 8 Aprili 2025 - 19:18
Tamko la Ja'miat Mudarsin, Hawza ya Qum kwa mnasaba ya kuharibiwa Makaburi ya Maimamu wa Baqi (a.s)

Hawza/ Ja'miat Mudarisin Qum, inatoa salamu za rambirambi kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya tukio la kuhuzunisha na la kusikitisha la uvunjiwaji heshima maeneo matukufu ya Maimamu watukufu wa Baqii rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, tukio ambalo lilifanywa na mawahabi wenye misimamo mikali ya kisalafi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Hawza, matini ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:

"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu atatimiza nuru Yake, hata kama makafiri watachukia." (Surat Swaf/8)

Mnamo tarehe 8 Shawwal mwaka 1344 Hijria Qamaria, mawahabi waliharibu makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), pamoja na kaburi la Bwana Hamza (a.s) huko Uhud. Pamoja na kubomoa makaburi ya Maimamu (a.s) pia ya yapo makaburi mwengine ambayo pia waliyaharibu, makaburi hayo ni pamoja na:
- Kaburi linalo nasibishwa na Bibi Fatimah Zahra (s.a)
- Kaburi la Fatimah bint Asad (s.a)
- Kaburi la Bibi Ummul Banin (a.s)
- Kaburi la Ibrahim mwana wa Mtume (s.a.w)
- Kaburi la Ismail mwana wa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s)
- Makaburi ya mabinti wa Mtume (s.a.w)
- Kaburi la Halimah Sa’diyah, mlezi wa Mtume (s.a.w)
- Kaburi la mashahidi wa enzi ya Mtume (s.a.w)

Mawahabi mnamo mwaka 1343 H.Q, huko Makkah walivunja Kuba ya kaburi la  Hadhrat Abdulmuttalib, Abu Talib, Bibi Khadija, na hata mahali alipozaliwa Mtume (s.a.w). Na huko Jeddah, walivunja kaburi la mama yetu Hawa pamoja na makaburi mengine kadhaa. Kuba ya kaburi tukufu la Mtume (s.a.w) waliiziba lakini kwa kuogopa hasira za Waislamu, hawakulivunja kaburi lake takatifu.

Mnamo Shawwal mwaka huo huo walipoharibu makaburi ya Baqii, walichukua vitu vyenye thamani kubwa vilivyokuwa katika makaburi hayo. Kaburi la Hadhrat Abdallah na A'mina wazazi wa Mtume (s.a.w) waliyaharibu, pamoja na kaburi la Bwana Hamza na mashahidi wengine wa Uhud pia waliyasambaratisha.

Katika mwaka huo huo walivamia Karbala, wakavunja sehemu ya kaburi la Imam Hussein (a.s), wakapora mali na vito vya thamani vilivyokuwa vimetolewa na wafalme pamoja na watu wenye heshima zao kwenye Kuba hizo. Katika uvamizi huo, takriban watu elfu saba waliuawa wakiwemo wanazuoni, masayyid, na raia wa kawaida. Baada ya hapo walijaribu kuvamia mji wa Najaf, lakini walishindwa na kulazimika kurudi wakiwa kapa.

Kwa mnasaba huu wa huzuni, Ja'miat Mudarisin  Hawza Qum, inatoa mkono wa pole na salamu za rambirambi kwa waislamu wote, wapenzi wa Ahlul Bayt (as), Mara'ji wa kiislamu "Mola awahifadhi", Kiongozi mkuu wa mapinduzi Ayatullah al-Udhma Imam Sayyid Ali Khamenei "Mwenyezi Mungu amlinde", na hasa kwa Imam Mahdi (a.j), huku tukimuomba Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na awaangamize maadui wote wa uislamu.

Majma Ja'miat Al-Mudarisin/ Hawza, Qom

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha